Diwani wa Kata ya Kia kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Yohana Laizer ameendelea kusota rumande baada ya hakimu anayesilikiza kesi yake kutokuwepo mahakamani, ikielezwa kuwa yupo likizo.

Diwani huyo anatuhumiwa kwa makosa mawili ya kumbaka na kumpatia ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi Obrieni iliyopo Kata ya Kia Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.

Aidha, kesi hiyo namba 152 ya 2018 ilipangwa kusikilizwa katika mahakama ya Wilaya ya Hai, lakini imeahirishwa kwa mara ya tatu kutokana na hakimu kutokuwepo mahakamani hapo.

Hata hivyo, hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Hai, Regina Mushi ambaye kesi hiyo kwa mara ya kwanza ilitajwa mbele yake, amesema kuwa hakimu mwenye mamlaka ya kusikilia kesi hiyo yupo likizo, kwamba yeye hana mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo mpaka pale hakimu huyo atakaporejea.

 

Ni lazima fedha hizi zikaboreshe miundombinu ya barabara- JPM
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 30, 2018