Mchezea santuli wa Clouds FM, DJ-D Ommy aka Mr. Washawasha anazidi kupanda ngazi za Kimataifa ambapo hivi karibuni ameachia kazi aliyomshirikisha DJ Walshy Fire wa kundi la Major Lazer.

D-Ommy ambaye ni mshindi wa tuzo ya D-J Bora Afrika ameachia mchanganyiko wa nyimbo (mixing) ambayo amemshirikisha DJ huyo Mjamaica anayetajwa katika orodha ya ma-DJ wakubwa zaidi wa kimataifa.

Mixing hiyo iliyobatizwa jina la #54 imebeba nyimbo kubwa za mahadhi tofauti ikiwa ni pamoja na nyimbo za Tanzania ambazo amezitambulisha zaidi kwa mashabiki wa muziki mzuri duniani.

“Hii mixing nimeiita #54 nikimaanisha nchi 54 za Afrika nikiendelea kujivunia kuwa Muafrika. Kwakweli kwangu ni hatua kubwa kushirikiana na DJ Walshy Fire wa Major Lazer na kazi yangu kuingia kwenye orodha ya Afro Carribean Mixx kubwa,” alisema Mr. Washawasha.

D-Ommy ameeleza kuwa mwimbaji Vanessa Mdee ndiye aliyemuunganisha na mtu wa karibu wa DJ Walshy Fire na mchakato huo kuishia katika kazi nzuri iliyofanyika.

Mr Washawasha amekuwa akitoa mix kadhaa zilizomjengea jina na ngome ya mashabiki waliomuwezesha kuonekana na kushinda tuzo kubwa barani Afrika.
Isikilize hapa #54:

Video: Waziri Mkuu atembelea kiwanda cha kampuni ya SBC Tanzania Ltd
August Alsina amaliza bifu na mama yake mzazi jukwaani