Ma DJ na wasanii wa muziki wa kizazi kipya hata Tanzania wametakiwa kutopenda kulalamika na kufanya kazi kwa muda mrefu kama wanatafuta mafanikio.

Ushauri huo umetolewa na DJ Mkongwe nchini aliekaa kwenye historia ya kiwanda cha burudani kwa muda mrefu anaefahamika kwa jina la Venture katika mahojiano na Dar24 Media.

Venture amesema wasanii wa Tanzania wanapenda kufuatilia midundo ya nchi nyingine na kusahau asili ya Tanzania huku akiwataka Ma DJ kufanya kazi ya kuwaburudisha wachezaji na sio wao pi kucheza.

DJ Venture katika Mahojiano na Harun Tambwe wa Dar24 Media
Wamachinga zimebaki siku mbili
Simulizi: Wanetu kukosa akili darasani kulivyohatarisha Ndoa yangu