Novak Djokovic amefanikiwa kushinda ubingwa wa tano wa Indian Wells na kuweka rekondi ya kuchukua mataji 27 ya Masters crown, baada ya kumchakaza mpinzani wake kutoka mjini California nchini Marekani  Milos Raonic, kwa seti mbili kwa sifuri ambazo ni  6-2 na 6-0.

Djokovic ambaye ndiye kinara wa ubora wa tennis kwa upande wa wanaume duniani, alionekana kutokutumia nguvu katika mchezo wake wa hatua ya fainali dhidi ya Raonic, kutokana na mpinzani wake kuonyesha alikua na jeraha la misuli ya paja.

Kwa ushindi huyo, Djokovic ameendelea kuweka rekodi mbele ya Roger Federer ambaye ameshawahi kutwaa ubingwa wa Indian Wells mara nne, na sasa bingwa huyo kutoka nchini Serbia anakwenda sawa na Rafael Nadal, kwa kutwaa taji la 27 Masters Crown.

Remi Garde Kufungasha Na Kurejea Nyumbani Ufaransa
Uchaguzi Zanzibar: Haya hapa matokeo ya majimbo kadhaa