Bingwa wa michuano ya US Open mwaka 2015, Novak Djokovic amesema kuna ulazima kwa mashabiki wa mchezo wa Tennis kuendelea kumuunga mkono kutokana na mafanikio anayoendelea kuyapata.

Djokovic anayeshika namba moja kwa ubora duniani upande wa wanaume, amezungumza maneno hayo siku moja baada ya kumshinda Roger Federer katika mchezo wa hatua ya fainali ya michuano ya US Open ambao ulishuhudia akishinda kwa seti tatu kwa moja ambazo ni 6-4, 5-7, 6-4 na 6-4.

Amesema anajihisi furaha kuona mashabiki wengi duniani wakiendelea kumuunga mkono, kutokana na wingi wao unao onekana uwanjani pamoja na katika mitandao ya kijamii kutoka katika kona zote duniani.

Kasi ya mashabiki kwa Djokovic iomeendelea kuongezeaka kutokana na juhudi kubwa aliyoionyesha kwa mwaka huu, na kufanikiwa kutwaa mataji matatu ya Grand Slam, kupitia michuano ya Australian Open, Wimbledon pamoja na US Open huku akitinga katika hatua ya fainali ya michuano ya French Open na kufungwa na Stan Wawrinka kutoka nchini Uswiz miezi miwiwli iliyopita.

Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa Djokovic kutwaa mataji matatu ya Grand Slam kwa mwaka mmoja, kwani aliwahi kufanya hivyo mwaka 2011, kwa kujishindia mataji ya Australian Open, Wimbledon pamoja na US Open.

Newcastle Utd Wachapwa Tena
Real Madrid Yashuka Viwango Vya Ubora Wa Thamani