Mlinzi wa kulia wa AS vita Club Shabani Djuma ameweka wazi mpango wa kufanya mazungumzo na viongozi wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC, ili kuangalia uwezekano wa kujiunga nao mwishoni mwa msimu.

Djuma ameamua kuweka wazi mpango huo, baada ya kuhusishwa na taarifa za kugoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kufanya kazi na AS Vita Club, huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Amesema baada ya mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, hatua ya makundi dhidi ya Simba SC uliocheza mjini Kinshasa mwezi Februari, baadhi ya viongozi wa klabu hiyo ya Tanzania walimfuata na kuzungumza naye.

“Ni kweli kuna baadhi ya viongozi wa Simba walinitafuta kwa ajili ya mzungumzo ya awali ya usajili lakini siwezi kulizungumzia sana hilo kwani sasa.

“Hii ni kwa sababu wote kwa sasa tunapambana kuzisaidia timu zetu zifanye vizuri katika michuano ya kimataifam ikizingatiwa tupo kundi moja.

Djuma amekua na kiwango bora ndani ya AS Vita Club, ambapo msimu huu katika michuano yote aliyoichezea timu hiyo amefunga mabao 6 na kutoa pasi tano za mabao.

Hata hivyo Djuma anaendelea kuwa sehemu ya kikosi cha AS Vita Club katika kipindi hikia mbacho wanashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, hatua ya makundi huku viongozi wa klabu hiyo ya DR Congo wakiendelea kumbembeleza ili asaini mkataba mpya.

Endapo ataendelea na msimamo wakutosaini mkataba mpya klabuni hapohadi mwishoni mwa msimu huu, beki huyo atakua huru kujiunga na klbu yoyote ndani ama nje ya DR Congo.

Kutokana na uwezo wa beki huyo, ni wazi endapo beki atafanikiwa kujiunga na Simba SC ataenda kugombea namba na Shomari Kapombe ambapo utakuwa mtihani mgumu kwa kocha kuchagua nani wa kuanza kulingana na ubora wa mabeki hawa.

Museveni akishtumu Chama cha Bobi Wine kuiba kura
Congo yaishtukia chanjo ya Corona