Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli amemteua Dk. Asha Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Dk. Migiro amechukua nafasi iliyoanchwa na Balozi Peter Kallaghe ambaye kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, Balozi huyo amerudishwa nyumbani.

Rais Magufuli anatarajia kumuapisha leo Dk. Migiro katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.

Wabunge wapigana ngumi bungeni
Ruvu Shooting Watangaza Msimamo Wao Wa Usajili