Rais Mstaafu wa Bunge la Afrika, Dk. Getrude Mongella, amesema kuwa kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais  magufuli, inamnyima usingizi kwa sababu huenda ikawaacha wanawake nyuma na kukosa haki yao.

Ameyasema hayo wakati akiwasilisha mada ya nafasi ya mwanamke katika Tanzania ya viwanda kwenye kongamano lililowakutanisha zaidi ya wanawake mia moja kutoka sehemu mbalimbali nchini lililopewa jina la Women Roundtable forum.

“Magufuli ana kasi ambayo msiokuwa na mbio mtapiga pua chini,akina mama mnalitazama hilo,mimi hili linaninyima usingizi,tukiachwa na mapinduzi haya tutakuwa wageni wa nani,nawaonea huruma wanawake wenzangu na ujuzi wenu”amesema Mongela.

Hata hivyo, Mongela ameitaka Serikali kuwaaandaa wanawake kitaaluma ili kuweza kushiriki kikamilifu katika uchumi wa viwanda bila kuwafanya wanawake wababaike na kupiga magoti ili wapate haki zao.

Wafuasi wa chadema kortini Karatu
Muhongo atoa siku 15 kwa mkandarasi kuunganisha umeme