Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango amesema kuwa hali ya uchumi hapa nchini inaendelea vizuri na kuongeza kuwa Shirika la Fedha la umoja wa mataifa pamoja na taasisi nyingine za utafiti zikiwemo, REPOA na ESRF zimesema uchumi wa Tanzania unakwenda vizuri.
Aidha, Mpango aliongeza kuwa hakuna taifa lisilo kuwa na changamoto ya uchumi na kwamba changamoto zilizopo ni za kawaida kama zilivyo katika nchi zingine.
Ameyasema hayo alipokuwa akifungua mkutao wa 18 wa siku mbili wa Benki kuu ya Tanzania unaoendelea jijini Dar es salaam.
Mpango ameziagiza taasisi za nchini kutoa mikopo kwa taasisi na mashirika madogo madogo ili yatumie jiografia ya nchi kwa kukuza uchumi katika sekta ya kilimo, biashara na madini na matumizi bora ya bandari kwaajili ya meli zitokazo mashariki ya mbali.