Rais wa Serikali ya Mapinduzi, Dk. Ali Shein amekanusha vikali tuhuma zilizotolewa na mgombea urais wa CUF, Maalim Seif Sharif kuwa amevunja makubaliano ya kubadili watendaji katika tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo (ZEC).

Akiongea baada ya kukamilisha utaratibu wa kurudisha fomu katika ofisi za ZEC, Dk. Shein alisema kuwa madai ya Shein si ya kweli kwa kuwa hawakukubaliana kubadili watendaji wa ZEC na kwamba hatafanya hivyo kwa kuwa watendaji waliopo wana sifa za kutosha.

Aliongeza kuwa CCM lazima itashinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu tena kwa kishindo na sio kwa kuiba kura kama anavyodai Maalim Seif, na kwamba ushindi huo utatokana na kazi nzuri iliyofanywa na chama hicho hivyo wananchi hawana budi kuendelea kukisapoti.

Dk. Shein alisisitza kuwa CCM ilishinda kwa haki katika uchaguzi mkuu uliopita na kwamba tuhuma hujuma sio za kweli.

Hivi karibuni, Maalim Seif alidai kuwa Dk. Shein amekiuka makubaliano ya awali kati ya vyama hivyo kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu, watabadili sekretarieti ya ZEC ili kuhakikisha kunakuwa na usawa na haki tofauti na ilivyokuwa katika uchaguzi uliopita ambapo anaamini alishinda lakini aliibiwa kura.

Arsenal Vs Liverpool Hakuna Mbabe
Zitto Kabwe Awashukia Wasanii Wanaopigia Debe Chama