Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanziabar, Dk. Ali Mohammed Shein ametengua kitendawili kilichokuwa kikisubiriwa cha iwapo kutakuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa visiwani humo katika awamu hii na uwepo wa Makamu wa Kwanza wa Rais.

Akitoa hutuba yake jana alipokuwa akifungua Baraza la Wawakilishi, Dk. Shein alisema kuwa hakutakuwa na Makamu wa Kwanza wa Rais pamoja na Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwakuwa vyama vya upinzani havikukidhi vigezo vya kujumuishwa kwenye serikali yake.

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010, ili chama kiweze kujumuishwa kwenye serikali ya umoja wa kitaifa lazima kifikishe angalau asilimia 10 ya kura zote, kigezo ambacho hakikufikiwa na vyama vya upinzania katika uchaguzi wa marudio.

Rais Shein alisema kuwa katiba inaeleza wazi vigezo vya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kwamba kutokana na ushidni wa kishindo alioupata, Wazanzibar wameamua kuwe na Serikali inayoongozwa na chama kimoja katika awamu hii.

Katika hatua nyingine, Rais Shein amewateua waliokuwa wagombea urais wa vyama vya upinzani kujumuka katika Baraza la Wawakilishi, akiwemo aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais wa chama cha ADC, Hamad Rashid Mohammed, Said Soud Said aliyewania nafasi ya urais kupitia AFP Wakulima na Juma Ali Khatib wa ADA-TADEA.

Katika awamu iliyopita, CUF ambao mwaka huu walisusia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 wakitaka mshindi wa uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 atangazwe, walijumuishwa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambapo Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais.

Dudu Baya alipuka tena, adai Bora Chidi Benz Afe
Al Ahly Yawasili Dar es salaam, Wajifanya Mabubu