Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa amesifia kasi ya rais John Magufuli hasa katika kupambana na ufisadi nchini.

Dk. Slaa amesema kuwa alichowahi kukizungumzia awali kimetimia kwa kuwa nchi hii ilihitaji mtu kama Magufuli.

“Nadhani sasa unaelewa niliposhikilia msimamo wangu. Katika mazingira ya sasa Magufuli ni bora zaidi. Niliwahi kusema kuwa hii nchi kwa siku za mwanzo inahitaji udikteta kuirudisha kwenye mstari ulionyooka, nimefurahi sana,” Dk. Slaa aliliambia gazeti la Raia Mwema.

Alisema kuwa Bunge linatakiwa kufanya kazi ya kuudhibiti udikteta huo ili usivuke mipaka lakini limuunge mkono kwa hatua anazochukua.

Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alimshauri rais Magufuli kuiangalia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kuifumua.

“Pasipo kuchukua hatua ya kuifumua Takukuru, sina hakika kama matarajio yatafikiwa,” alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa hatua hizo zinapaswa kuchukuliwa haraka.

Tajiri Anayemiliki Makontena Yaliyopotea Bandarini Ajitokeza, Afunguka
Kafulila Aanza Vizuri Kesi Yake Ya Kupinga Matokeo