Wakati ambapo vyama vya upinzani vinatarajia kuzindua kampeni zake katika uwanja wa Jangwani kesho na kumnadi mgombea wake wa urais, Edward Lowassa, duru zinaeleza kuwa huenda Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa akahudhuria uzinduzi huo.

Mmoja kati ya viongozi wa Chadema ambaye alinukuliwa na gazeti la Majira huku akitaka jina lake lisitajwe, alisema kuwa zipo taarifa za chinichini ndani ya chama hicho zinazoeleza kuwa Dk. Slaa ataibuka Jangwani kesho.

“Zipo taarifa za chinini kuwa Dk. SSlaa atahudhuria uzinduzi, hatujui zina ukweli kiasi gani na atashiriki kama Katibu Mkuu au mgeni mwalikwa, kama atahudhuria, atatusaidia sana na asipokuja suala lake litaendlea kuwachanganya wafuasi wa Chadema,” alinukuliwa kiongozi huyo wa Chadema.

Haijafahamika kama taarifa hizo ni za kweli au la kwa kuwa hata uamuzi wa kumkaribisha Edward Lowassa kujiunga na Chadema ulifanywa kuwa siri kubwa kwa viongozi wachache sana takribani miezi mitatu kabla. Hata viongozi wengine wa ngazi za juu walikuwa hawajui kabisa kinachoendelea.

Dk. Slaa alijiweka kando na harakati za kampeni za Chadema na Ukawa kwa ujumla baada ya kutoridhia uamuzi wa chama chake kumkaribisha Edward Lowassa ambaye awali walikuwa wanamtuhumu kuwa katika orodha ya mafisadi wakubwa nchini.

Ukawa wanatarajia kufanya uzinduzi wao kesho (Agosti 29) katika viwanja vya Jangwani ikiwa ni wiki moja baada ya CCM kuutumia uwanja huo kwa shughuli hiyohiyo.

Magufuli: Peoples Power, Nipeni Power Nilete Mabadiliko
Ukawa, CCM Wagombea TV Kurusha Matangazo ‘Live’ Jumamosi Hii