Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa ameeleza kunasa mpango wa nchi za Ulaya kuiingiza Tanzania katika orodha ya nchi hatari kwa uwekezaji (Risky investiment destination).

Dk. Slaa ambaye hivi sasa anaishi nchini Canada, ameliambia gazeti la Mtanzania mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa endapo Tanzania itaingia kweli katika orodha hiyo itaathirika hususani katika sekta ya mafuta na gesi; biashara na utalii.

“Mwenendo wa biashara na sekta ya utalii vinaweza kurodorora hatimaye kuwa ghali sana,” alisema.

Hata hivyo, Dk. Slaa alieleza kuwa kunyimwa misaada na wahisani kusiiogopeshe nchi bali iwe chanzo cha kuanza kutafuta jinsi ya kujitegemea na kwamba kwakuwa wao pia wanahitaji rasilimali zetu, watarudi wenyewe bila kubembelezwa na hapo ndipo tutakapoheshimiana.

“Wao pia wanahitaji rasilimali tulizonazo, ni suala la muda tu. Watarudi wenyewe bila kubembelezana. Watakaporudi tutaheshimiana kwa kuwa wakati huo na sisi tatakuwa tumejenga uwezo wetu,” alisema Dk. Slaa alipokuwa anatoa maoni yake kuhusu MCC kuinyima Tanzania mabilioni.

597 Waliofutwa kazi NIDA kupata 'chao'
Haji Duni akosoa Muundo wa Chadema