Dk Tulia Ackson amekanusha madai ya baadhi ya watu kuwa amepandikizwa na serikali kuwa Naibu Spika wa Bunge la 11 ili aibebe na kuirahisishia kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Dk Tulia ambaye alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kabla ya kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa mbunge na leo anagombea nafasi ya unaibu Spika, amesema kuwa madai hayo hayana msingi na kwamba ameteuliwa kutokana na sifa alizonazo.

alisema kuwa akiwa Naibu Spika atafanya kazi ya Bunge kwa mujibu wa sheria na sio kazi ya kumsaidia serikali kama inavyodaiwa.

“Ni kweli nimeteuliwa na Rais, lakini nakwenda kufanya kazi ya Watanzania. Nikipata nafasi ya kuwa Naibu Spika hayo madai kuwa nitaibeba serikali hayana msingi. Nitafanya kazi za Bunge ambazo ni kuisimamia, kumshauri na kuiwajibisha serikali,” ananukuliwa.

Tulia atachuana na mgombea wa CUF anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Ukawa, Magdalena Sakaya ambaye ni mbunge wa jimbo la Kaliua.

Kura za wabunge wengi zitaamua kati ya wagombea hao ni nani awe Naibu Spika.
Hata hivyo, Dkt Ntulia ana nafasi kubwa zaidi ya kuchaguliwa kutokana na Bunge hilo kuwa na idadi kubwa ya wabunge wa CCM.

Vilio vyatawala bomoa bomoa Dar
Magufuli amteua Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu