Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas amesema kuwa ahadi ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya kutoa milioni 50 kila kijiji itatekelezwa ingawa chama hicho hakikutaja wakati maalumu wa kutoa pesa hizo.

Amesema kuwa upo utaratibu ambao utawekwa ili ahadi hizo zitekelezwe ingawa anaamini kuwa serikali imefanya mambo makubwa zaidi ya milioni 50.

“Mimi ukiniuliza utekelezaji, serikali imeshafanya mambo makubwa kuliko milioni 50 hizo. Mtu akisema haoni kitu haitendei haki nchi yetu. Maji si yanakuja, barabara si zipo madawa pia. sasa kama wewe ulikuwa unasubiria hizo milioni 50 kwa ajili ya kupiga dili tulia kwanza,”amesema Dkt. Abbas

Hata hivyo, Serikali iliyopo madarakani kupitia Chama Cha Mapinduzi wakati wa uchaguzi mkuu 2015 chini ya Rais John Pombe Magufuli iliahidi kugawa milioni 50 kwa kila kijiji ahadi ambayo mpaka sasa inaonekana kutotekelezeka.

 

Mahakama yamnyeshea aliyemuua mwanamke kwa ngumi moja
Odinga azungumzia kumtoa Kenyatta Ikulu