Mkurugenzi wa Idara Habari( MAELEZO) Dkt. Hassan Abbas ameanza ziara ya kutembelea vyombo vya habari Mkoani Dodoma kwa lengo la kuona na kujua changamoto za kiutendaji pamoja na jinsi gani wamejipanga juu ya Serikali kuhamia Dodoma.

Akiwa katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Abbasi amevitaka vyombo vya habari vya Dodoma kuwa tayari na ujio wa Serikali kuhamia Dodona kwani matukio mengi ya kiserikali yatafanyika Mkoani humo.

“Kwa baadhi ya matukio yaliyofanyika hapa Dodoma nimeona uzubaifu kwa baadhi ya waandishi wa habari hivyo wanahabari wenzangu tuchangamke kwani matukio mengi ya Serikali yatafanyika hapa” amesema Dkt. Abbas

Aidha, ameutaka uongozi wa TSN kufuata maadili katika utendaji kazi kwani wananchi hutazama kampuni hiyo kwa jicho la utofauti kama chombo cha Serikali.

Akiwa katika Ofisi za Mwananchi Communications Ltd mkoani humo, Dkt Abbasi amesema kuwa asilimia 99 ya waandishi wamejikita katika masuala ya kisiasa kuliko masuala ya maendeleo ya nchi au bajeti mbalimbali zinazohusu serikali hivyo ameshauri vyombo vya habari kujikita zaidi katika masuala ya maendeleo kwa manufaa ya jamii.

Hata hivyo, amewasisitiza waandishi wa habari kujisajili ili wapatiwe vitambulisho (Press Card) kwani kuanzia mwezi Machi mwaka huu katika matukio yote ya viongozi wakuu wa Kitaifa kila mwanahabari atatakiwa kuwa na kitambulisho hicho.

Video: Makamu wa Rais asisitiza utunzaji mazingira
Young Africans washindwa kutamba nyumbani