Msemaji mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameona falsafa na njia alizozitumia aliyekuwa Rais John Pombe Magufuli hivyo tutatumia njia hizo kufanikisha ndoto za Hayati Magufuli.

Dk Abbas ameyasema hayo leo katika uwanja wa Magufuli wilayani  Chato ambapo wananchi wa Wilaya hiyo na maeneo jirani wanatoa heshima za mwisho kwa kiongozi huyo aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo Machi 17, 2021.

“Kwa kujikusanya tukafanya vitu vingi, tuahidi viongozi tunaendelea chini ya Mama Samia na viongozi wengine sisi ni wanafunzi wazuri wa Magufuli tumeona maono yake, falsafa zake  njia zake alizokuwa anazitumia kufanikiwa kutekeleza, kwa hiyo naamini kwa dhati chini ya Rais Samia tutafanikiwa kufanya yale ambayo yeye ilikuwa ndoto yake, aliyaanza tutatekeleza miradi yote mikubwa.” amesema Abbas

Amesema Magufuli alikuwa mtu wa maono na mtekelezaji makini na mahiri na  nchi inamshukuru ameweka misingi na kufanya mambo makubwa ya maendeleo yanayogusa watu kwa kutumia fedha za ndani.

“Kila eneo bahati nzuri ameacha wanafunzi wazuri waliomuelewa ambao ni watekelezaji pia chini ya mama Samia na kwa kuwa alikuwa mbunifu na sisi tumekuwa wabunifu. Watanzania tuendelee kumuombea, kuna watu wanatumwa duniani kuja kuwa rehema waipeleke nchi kutoka eneo moja kwenda jingine kwetu sisi Tanzania Magufuli ni mmojawapo,” amesema Abbas.

Amesema viongozi wote wa Serikali wajue wana deni la kuendeleza yale mazuri yote na kwamba miradi yote itatekelezwa.

Tshishimbi: Tutaifunga Simba kwa Mkapa
Taifa Stars kucheza bila mashabiki