Baada ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusikika wakidai vyombo vya usalama kutoka nje ya nchi vije kufanya uchunguzi wa shambulio la MbungeTundu Lissu, Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas amehoji watu wangapi wamekufa wilayani Kibiti na wazungu hawakuja kuchunguza.

Dkt. Abbas Kupitia ukurasa wake wa twitter amehoji kwa kuandikaWaje wazungu? Wamekufa watu wangapi Kibiti hatukuita wazungu?Lakini hatujui pia hata hao wazungu kwao makosa ya jinai pia yamewazidi nguvu?

Aidha, Dkt Abbas ameongeza kuwa tabia ya kutuhumiana kunapotokea kosa la jinai ambalo limetendwa kwa mtu yoyote au mwanasiasa siyo vizuri kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha mtu mwenyewe akawa mshukiwa namba moja wa tukio.

“Ni busara vyombo vya dola vikaachwa vifanye kazi yake kwanza na siyo kutuhumu wakati upelelezi unaendelea kufanywa,”ameongeza Dkt. Abbas

Hata hivyo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo kupitia viongozi wake wamekuwa wakitaka serikali iruhusu vyombo vya kimataifa kuja nchini kufanya uchunguzi juu ya shambulio la Tundu Lissu aliyepigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 akiwa nje ya nyumba yake Area D’ Dodoma.

 

Magazeti ya Tanzania leo Septemba 23, 2017
Mbowe ashangazwa na kauli ya Waziri Ummy, Spika