Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally amewataka vijana nchini kuchangamkia fursa ya elimu ili wapate ujuzi na maarifa ya kulinda na kusimamia rasilimali za nchi yao zisiporwe.

Ameyasema hayo katika ziara yake ya kujitambulisha visiwa Zanzibar wakati akizungumza na vijana kutoka makundi mbalimbali ya Umoja wa vijana wa CCM (UVCCM).

Amesema kuwa elimu ndio njia pekee ya kuwajenga vijana wa CCM kuwa na fikra chanya za kulinda tunu za taifa lao zisihujumiwe bali ziendelezwe kwa lengo la kuvinufaisha vizazi vya sasa na vijanavyo.

Dkt. Bashiru amesema kuwa vijana waliopikwa kiitikadi na kurithishwa siasa za ukombozi na ulinzi juu ya misingi ya kitaifa, wanakuwa madhubuti katika kuendeleza kazi katika nyanja mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kisiasa.

“Vijana hamuwezi kulinda Mapinduzi ya Zanzibar wala azimio la Arusha bila kujielimisha juu ya historia ya taifa lenu ambalo ndio chimbuko la vuguvugu la ukombozi wa nchi mbalimbali za bara la Afrika.”amesema Dk.Bashiru.

Hata hivyo, ameongeza kuwa milango ya Tanzania ipo wazi kwa mataifa yanayotaka kuja kujifunza demokrasia hapa nchini kwani mfumo huo unazidi kuimarika kila kukicha.

 

 

Lugola aonya Polisi kutumiwa na mafisadi
Video: Makonda, Nape wavaana wapinzani kuhamia CCM