Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt. Bashiru Ali amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho, kufuta ndoto walizokuwa nazo za kutaka kushika madaraka ya urais wa Zanzibar licha ya kuwa mhusika yupo na muda wake haujakwisha kwa mujibu wa sheria.

Ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM visiwani Zanzibar katika ziara yake ya kazi baada ya kusikia tetesi, kuwa kuna baadhi ya viongozi wa CCM wameanza kuunda makundi yenye lengo la kutaka kumtoa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein.

“Wapo watu nasikia wengine wana vyeo na wengine hawana, wana ndoto ya kushika madaraka ya urais wa Zanzibar hiyo nafasi haijatangazwa kuwa wazi bado ina mwenyewe. CCM sio chama cha kusaka vyeo ni chama cha mapinduzi, wafuata vyeo ‘wakome’. Tutaendelea kuwafuatilia wengine tunawajua na siku zenu zinahesabiwa. Muacheni Rais Shein amalize kipindi chake kwa heshima. Wakati ukifika tutasema na kuweka utaratibu,”amesema Dkt. Bashiru.

Hata hivyo, Dkt. Bashiru ameongeza kuwa kama nafasi hiyo itakuwa wazi basi wataitangaza kwa mujibu wa sheria kufuatana na chama chao kinavyosema na sio kupitia makundi ya watu yanayoendelea mahotelini.

 

Habari Picha: Rais Dkt. Magufuli amjulia hali Dada yake aliyelazwa hosptali ya Bugando
BREAKING: Rais Magufuli akiongea na Wananchi Sengerema