Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Gharib Bilal amewataka watanzania wanaosafiri kwa magari nchini kuacha tabia ya kujisaidia vichamani/porini wanapokuwa safarini kwa kuwa vinaanzishwa vituo maalum vya kupumzika na kupata ‘faragha’.

Dkt. Bilal alisema hayo hivi karibuni alipokuwa akizindua na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa vituo vya mapumziko na vyoo vya wasafiri katika barabara kuu nchini, tukio lililofanyika katika kijiji cha Idetero, Wilayan Mufindi, Iringa.

Makamu huyo wa rais alisema kuwa mradi huo utasaidia kujengwa vituo vikubwa 44 vya abiria katika barabara kuu ili wasafiri waweze kupumzika na kupata faragha wanapokuwa njiani  na kuondokana na adha ya ‘kuchimba dawa’ vichakani/porini.

Msechu Adai Kupata au Kukosa Tuzo Sio ‘Ishu’
Azam FC Wadhamiria Kulipiza Kisasi