Mbunge wa Jimbo la Busega kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Raphael Chegeni amekabidhi vifaa mbalimbali kwaajili ya ukamilishaji wa majengo ya Zahanati na vyumba vya madarasa ili kusaidia upatikanaji wa elimu bora na huduma bora za afya katika wilaya ya Busega.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya mbunge, Katibu wa mbunge huyo, Timothy Mayala amekabidhi vifaa vya kusaidia kujifungulia akina mama (Delivery Packs), mashuka, Pampas, Vitanda vya hospitali 16, katika Zahanati ya Nyamikona, Mwanhale, Hospitali ya Mkula, Badugu, Ngasamo, Ijitu, Mwamigongwa, kituo cha afya Igalukilo na Zahanati ya Shigala.

Katika kuhakikisha huduma za kijamii zinaimalika, pia amekabidhi mifuko ya Simenti 50 kwaajili ya Shule ya Msingi Lamadi, Shule ya Msingi Mwabayanda mifuko 50 na Nondo 28, Shule ya Msingi Mwanhale mabati 100 ili kuweza kukamilisha uezekaji wa madarasa mawili, pia mifuko 50 ya simenti kwaajili ya ukamilishaji wa ofisi ya serikali ya kijiji cha Mwasamba.

Aidha mbunge huyo amekabidhi pia mifuko ya simenti 100 katika kijiji cha Imalamate, Nyangoko mabati 100, Busami Mabati 100, Bunyanyembe  simenti mifuko 26, Mwamkala simenti mifuko 26 pamoja na Ujenzi wa Zahanati ya Yitwilima A ambapo amekabidhi simenti mifuko 100 pamoja na ukamilishwaji wa maboma 2 ya shule ya msingi Milambi amekabidhi mabati 100.

Hata hivyo, hizo zote ni ahadi za mbunge huyo alizozitoa wakati wa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuunga mkono jitihada za wananchi katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi katika jimbo la Busega.

  • Rais Magufuli kufanya ziara ya siku 2 mkoani Njombe
  • Wahamiaji 12 wakamatwa mkoani Njombe
  • Video; Ziara ya Rais Magufuli mkoani Ruvuma

 

 

 

Vifo vyaongezeka Mafuriko Iran
Video: Bunge labariki msajiri kuvishughulikia vyama, JPM akerwa na Wizara ya Maji