Waziri wa Afya Mendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto Dkt Doroth Gwajima amesema kuwa matumizi ya takwimu zenye ubora katika halmashauri nchini bado ni changamoto hali ambayo inarudisha nyuma sekta ya afya.  

Ameyasema hayo leo September 7,2021 wakati wa madhimisho ya siku ya Epidemiology Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere square Dkt.Gwajima  amesema kuwa ili kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa na matukio yanayoathiri afya ni vema kutambua mapema viashiria hatari.

Katika jamii yetu ni lazima pawepo na takwimu zenye ubora katika ngazi ya halmahauri jambo litakalo saidia kuinua sekta ya afya, ” Amesema Dkt Gwajima.

Aidha Dkt.Gwajima ameeleza kuwa jumla ya watumishi 512 kutoka idara ya afya ya binadamu na idara ya afya ya mifugo wamepatiwa mafunzo katika ngazi ya kozi ya awali kutoka mikoa yote 26 na halmashauri 159 kwa kipindi cha miaka sita.

Kwa upande wake Rais wa Umoja wa Field Epidemilojia Tanzania (TANFLEA) Dkt Elibariki Mwakapeje amesema kuwa wao kama TANFLEA ni kuhakikisha afya ya mtanzania inaimarika ili watu waweze kuwa na afya bora ili aendelee kufanya shughuli zao za kila siku.

Madhimisho ya siku ya Epidemiology yamefanyia kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kuadhimishwa siku ya wataalamu wa epidemiolojia na maabara ambao ndiyo makachero wa magonjwa yote ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza ili kutambua visababishi vya magonjwa na jinsi magonjwa yanavyo sambaa kwenye jamii .

Hata hivyo madhimisho hayo yamebebwa na kauli mbiu isemayo kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa na matukio yanayoathiri afya ili kutambua viashiria hatari kwa jamii.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 8, 2021
Mpango amuwakilisha Rais Samia Africa- CARRICOM Summit