Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima, amewataka wananchi kutofanya mzaha juu ya janga la corona kuwataka kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya janga hili.

Ameyasema hayo leo Julai 23, 2021 wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema si vema kila siku kutoa tathimini za wagonjwa waliokufa na waliopo badala yake kila mwanachi achukue tahadhari ili kunusuru afya na uchumi wa nchi.

“Nawakumbusha wanaoendelea kufanya mzaha na corona, wasifanye mzaha na UVIKO-19 na tusichukulie wa wepesi kuwa wimbi la kwanza na la pili lilipita, mimi nipo na huyu yupo, wapo wenzetu wengi walipita ukabaki wewe kwa kusudi la Mungu,” amesema Dkt. Gwajima. 

“Na hata leo wapo waliopita na jana wapo waliopita, tusichukulie kwa wepesi jamii ya virusi vinavyozunguka inabadilika sana na inatofautiana makali ya kushambulia hivyo tusiipe miili yetu kazi ya ziada,” amesema Dkt. Dorothy Gwajima.

“Wapo baadhi ya viongozi wanopambana na janga hilo, wapo baadhi ya viongozi ambao wamejitoa kiani hawafanyi vizuri wanakasi ndogo kusimamia kuwasaidia wananchi washinde vita, watu wasifanye mzaha.” amesema Dkt. Gwajima.

Anna Mghwira kuzikwa Julai 26
Mitungi zaidi ya gase inahitajika - Prof. Masenga