Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, (LHRC) Dkt. Hellen Kijo Bisimba amestaafu rasmi nafasi hiyo mara baada ya kuitumikia kwa muda wa miaka 22.

Dkt. Bisimba anastaafu rasmi wadhifa huo June 30 huku akiacha historia kubwa katika taasisi hiyo inayojishughulisha na masuala ya haki za Binadamu.

Aidha, LHRC imemteua Anna Henga kuwa mkurugenzi mkuu wa kituo hicho na ataanza rasmi majumu yake julai mosi mwaka huu.

Dkt. Bisimba amesema kuwa anajivunia jambo moja kubwa ambalo amelifanya la kuwafanya watu watambue nini maana ya ‘Haki’

“Hapo awali watu walikuwa hawajui nini maana ya haki, tulipokuwa tunaanza ukimwambia mtu masuala ya haki hakuelewi unamaanisha nini,”amesema Bisimba

Hata hivyo, ameongeza kuwa aliomba kuondoka kwenye nafasi hiyo tangu mwaka 2011 lakini alibaki katika nafasi hiyo kutokana na maombi ya bodi ya kituo hicho.

Mugabe hatiani kuswekwa jela
Hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho- Kinana

Comments

comments