Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei amemwaga chozi hadharani wakati wa uzinduzi wa tawi la benki hiyo Wilayani Chato mkoa wa Geita mara baada ya wanahisa wa benki hiyo kumuomba aendelee baada ya muda wake wa uongozi kumalizika.

Akizungumza katika uzinduzi wa tawi hilo, Dkt. Kimei aliwajulisha Wanahisa hao kuwa muda wake wa kuongoza unamalizika Mei 31 mwakani.

Aidha, baada ya kuwajulisha Wanahisa hao kuwa mkataba huo unaisha, wameomba aongezewe muda wa kufanya kazi ili aweze kuinusuru benki hiyo.

Kwa upande wake, Askofu wa Kanisa la Furaha Tanzania, Jonas Molla amesema kuwa wanaomba Dkt. Kimei abaki kwenye benki hiyo kwa muda wa miaka mitano mingine.

“Kama Rais Dkt. Magufuli amekupongeza kwa kazi nzuri, kwanini sisi tukuruhusu uondoke, sisi ndio wanahisa wenye benki hii tunakuomba ubaki,”amesema Askofu Molla

Vardy aingia kwenye rada za Atletico Madrid
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike  Ureno