Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadala ‘Mabodi’ amewaagiza viongozi wa Serikali za Mitaa Zanzibar kuacha tabia ya kuruhusu uuzaji wa viwanja na ujenzi katika maeneo hatarishi hasa mabondeni ili kuepuka athari za mafuriko.

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Mjini Magharibi yaliyoathiriwa na na  mvua zinazoendelea kunyesha visiwani Zanzibar huku baadhi ya wananchi wakikosa pa kuishi.

Amesema kuwa wananchi wanatakiwa kujenga utamaduni wa kujilinda dhidi ya maisha yao kwa kuchukua tahadhari ya kutoishi katika maeneo wanayojua kuwa ni hatarishi juu ya afya na maisha yao.

“ Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi natoa pole sana kwa wananchi wetu wa Zanzibar kwa Unguja na Pemba walioathiriwa na mvua hizi zinazoendelea kunyesha hivi sasa, kwa upande wa CCM tutaendelea kuwa nanyi kwa kutoa msaada wa Ari na Mali ili kuhakikisha mnarudi katika hali yenu ya kawaida,”amesema Mabodi

 

Video: Nape, Kitwanga wageuziwa kibao, Wabongo kuitwa ajira A. Kusini
Magazeti ya Tanzania leo Mei 12, 2017