Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala  ‘Mabodi’  amewataka viongozi wa kisiasa wa chama hicho waliopewa dhamana ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015/2020 kwa wananchi waanze kujitathimini mapema kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Ameyasema hayo katika hafla ya utekelezaji wa Ilani hiyo iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Donge, Sadifa Juma  katika jimbo hilo huko Kaskazini “B” Unguja.

Dkt. Mabodi amesema kuwa viongozi wa kisiasa waliochaguliwa na wananchi kuanzia ngazi za Madiwani, Wawakilishi, Wabunge na Rais wa Zanzibar  kuwa utaratibu wa kubuni na kutekeleza miradi ya maendeleo sambamba na kuimarisha miradi ya huduma za kijamii sio suala la hiari bali ni lazima kwa kila aliyetumia tiketi ya chama hicho kuomba  ridhaa ya kuwatumikia wananchi.

“ Njia pekee ya CCM kubaki madarakani ni kutatua kero za wananchi mijini na vijijini bila kujali itikadi za kisiasa na kidini ili jamii endelee kujenga imani na upendo wa kudumu kwa Chama kilichoiweka serikali madarakani”, amesema Dkt. Mabodi.

Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu huyo Dkt. Mabodi ametoa ahadi ya shilingi 300,000 kwa skuli ya maandalizi Mkataleni pamoja na kusaidia ujenzi wa vyoo vya skuli hiyo ili watoto waweze kusoma katika mazingira bora.

 

Chadema Waifuata CCM Dodoma, Wapanga Kuteta haya
?Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Mei 25, 2017

Comments

comments