Pamoja na jitihada za Serikali za ujenzi wa nyumba za makazi zenye gharama nafuu bado kumekuwa na malalamiko kwa baadhi ya wananchi wanaodai kushindwa kumudu hitaji hilo kutokana na gharama za juu.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula wakati akifungua Mkutano wa siku mbili wa Wadau wa Sekta ya milki Tanzania, ulioanza hii leo Septemba mosi, 2022 jijini Dar es Salaam.

Mkutano wa wadau wa sekta ya Milki Tanzania.

Amesema, sulala hilo linapaswa kuangaliwa kwa umakini kwani linawafanya watu wengi kudhani kwamba Serikali haiwasaidii kitu ambacho ni kinyume kwani hujiridhisha kulingana na aina na ubora wa nyumba kabla ya kupanga bei husika.

Amesema, “Mtu anasema hizi nyumba zina gharama kubwa lakini swali la kujiuliza ni je analinganisha kwa mtazamo upi, maana lengo la serikali ninkutaka watu wake wishi katika nyumba bora sasa katika eneo hili ni vyema pia wadau mkaja na maoni katika mjadala wenu.”

Waziri Dkt. Mabula ameongeza kuwa, Serikali inalenga kuwawezesha wananchi kuwa na makazi bora yaliyo katika hadhi kama inavyokusudiwa na Wizara na kwa mujibu wa sera na ilani ya CCM katika miradi ya kimaendeleo.

Mkutano wa wadau wa sekta ya Milki Tanzania.

Amesema ujenzi huo unatarajia kuendana na uwepo wa huduma mbalimbali za kijamii za kimiundombinu ikiwemo barabara, maji vituo vya afya kwa kuweka jitihada za  kufanikisha mikakati iliyokusudiwa.

“Tutahakikisha pia tunaanzisha mikopo ya nyumba kupitia sera wezeshi zilizowekwa na Serikali ili kuwa na uendelezaji wa milki kwa taasisi zilizopo ambazo sitasimamia zoezi zima la kuwainua Watanzania kuwa na makazi bora,” amesema Dkt. Angeline.

Aidha, Waziri Mabula ameongeza kuwa upo umuhimu wa kuwekeza katika sekta ya milki na kufanya maboresho katika baadhi ya sheria nchini ili kuwa na sera ya nyumba yenye mazingira rafiki kwa wawekezaji na kuwafanya watu wengi kuishi katika nyumba za gharama nafuu.

“Kutokana na jitihada hizi sasa kuna ongezeko la miradi na sisi ni mashuhuda wa ujenzi unaoendelea kufanywa na mashirika mbalimbali ikiwemo NSSF, NHC na mengineyo yenye lengo la kuziwezesha jamii kuwa na makazi bora,” amebainisha Dkt. Mabula.

Awali, akiongea katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Allan Kijazi amesema Wizara inakusudia kufanya maboresho ya kisera, kisheria na kimkakati.

Amesema, kusudio hilo pia linalenga kuhakikisha wanafikia mahitaji yaliyokusudiwa na Sekta ya milki nchini na kuibua changamoto na mikakati mipya itakayosaidia kusonga mbele.

Mingange aipongeza Simba SC safari ya Sudan
UN: Ubaguzi kwa Waafrika bado ni tatizo