Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC), leo  imewakabidhi rasmi Dkt. John Magufuli na Bi. Samia Saluhu vyeti vya ushindi vinavyohalalisha kuwa Rais na Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tukio lililofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alianza kumkabidhi Dkt. John Magufuli cheti cha kumtambulisha kuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania na kusoma maandishi yaliyoandikwa kwenye cheti hicho. Alifanya vivyo hivyo kwa Bi. Samia Suluhu.

Tukio hilo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Rais anayemaliza mhula wake, Dkt. Jakaya Kikwete, Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na viongozi wengine wakubwa wastaafu. Rais wa zamani wa Nigeria, Goodluck Jonathan alikuwa miongoni mwa waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi waliohudhuria tukio hilo la kihistoria.

Ramires Akubali Kumuokoa Mourinho
Muamuzi Afungiwa Chumbani