Aliyekuwa Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dkt. Vicent Mashinji leo Jumanne Februari 18, 2020 amehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole.

Dkt. Mashinji amejiunga na CCM katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam, ambapo ni miezi miwili imepita tangu ufanyike mkutano mkuu wa Chadema na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kutompendekeza tena kuwa Katibu Mkuu.

Baada ya kukosa nafasi hiyo Dkt. Mashinji ameeleza masikitiko yake na kwamba alitamani kuwa katibu mkuu ili aweze kumalizia mipango aliyokuwa nayo, ikiwemo maandalizi ya uchaguzi mkuu 2020

”Nimemuomba Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli kama ataridhia anipe nafasi ya kujiunga na CCM iliniweze kuchangia maendeleo ya nchi yangu” amesema Dkt. Mashinji

Aidha katika mkutano mkuu ulifanywa na Chadema Mbowe alimpendekeza mbunge wa kibamba John Mnyika kuwa katibu mkuu wa tano wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Sauda Mwilima asimulia Meneja wa Diamond alivyomdanganya, ‘Diamond alikuja na begi’
Castle Lite Unlock kufungua milango ya tiketi Februari 20 kwa punguzo, msanii mkubwa wa hip hop Afrika kutumbuiza

Comments

comments