Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Vicent Mashinji amesema kuwa wametumia siku mbili kutafuta viwanja kwa ajili ya kuaga mwili wa kada wao maarufu aliyekuwa kwenye timu ya kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Kinondoni, Richard Hiza Tambwe lakini wamenyimwa.

Ameyasema hayo wakati wa kuaga mwili wa Richard Tambwe nyumbani kwa marehemu Mbagala jijini Dar es Salaam na baadae kwenda kupumzishwa katika makaburi ya Chang’ombe.

“Tumetumia siku mbili tunazunguka kutafuta viwanja ila kila sehemu ukigusa wanasema CHADEMA siasa, baadae mpaka kikao cha jana jioni tumekaa hapa na kaka zangu tukasema lakini huyu si alikuwa na nyumbani kwake? Sasa hata hapa nyumbani watatuambia ni siasa? Sasa huu ni ustarabu mpya tunaanza kufundishwa katika Taifa letu, ustarabu wa kuanza kuogopana, ustarabu wa kuanza kupeana makundi kwamba huyu ni wao sisi ni sisi,”amesema Dkt. Mashinji 

Hata hivyo, ameongeza kuwa wiki tatu zilizopita alimwita Tambwe ofisini kwa ajili ya kutaka kumtumia kuwa katibu muenezi kwenye uchaguzi mdogo wa marudio Jimbo la Kinondoni.

 

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 11, 2018
Baada ya kunyimwa uwanja, Yanga kukarabati uwanja wake