Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vincent Mashinji na viongozi wengine watatu wa chama hicho wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Hai, Mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usio halali.
 
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Hai ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo, Lengai Ole Sabaya ambapo amesema kuwa viongozi hao wamekamatwa mchana kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usiokuwa halali.
 
“Ni kweli tumemkamata Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Mashinji, katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Basir Lema, mwenyekiti wa halmashauri ya Hai, Egra Mchomvu na msaidizi wa mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, Irine Lema kwa kufanya mkusanyiko usio halali,” amesema.
 
Amesema kuwa viongozi hao, wamekutwa wakifanya mkusanyiko katika eneo la Boma bila ya kuwa na kibali jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
 
Aidha, Sabaya amesema katika wilaya yake ya Hai kwa sasa hataruhusu mikutano isiyo halali ambayo inalenga kuwapotosha wananchi kuhusu kazi nzuri ambazo zinafanywa na Rais Dkt. John Magufuli.
 
  • Kikokotoo chamuibua tena Bulaya, ‘Bora mjiuzulu’
  • JPM amtumbua Mkurugenzi aliyetetea kikokotoo cha 25%
 
  • Kanyasu atoa maagizo mazito wilayani Buchosa
 
Hata hivyo, baadhi ya wanachama wa Chadema wilaya ya Hai wamekiri kukamatwa kwa viongozi hao majira ya mchana hata hivyo hawakuwa tayari kufafanua chanzo cha kukamatwa kwao
HapoKale: Wachaga na kisa cha kurudi nyumbani kila mwisho wa mwaka
Tanesco yatoa neno kuhusu kukatika kwa umeme