Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, leo Julai 24, 2021 ameshiriki misa ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha hayati Rais wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa iliofanyika  Kijiji cha Lupaso Wilaya ya Masasi, huku

Akizungumza baada ya misa, Makamu wa Rais Mpango aliiwasilisha ujumbe Kutoka kwa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa wanamasasi na akaisoma nukuu hiyo ya Rais Samia.

“Nakutuma uwapelekee salamu zangu za upendo wanafamilia, wanalupaso, ndugu na jamaa na marafiki na wananchi kwa ujumla nawahakikishia kuwa serikali itaendelea kumuenzi baba yetu na kiongozi wetu Hayati Benjamini Wililiam Mkapa,” Alisoma Makamu wa Rais Mpango.

Makamu wa Rais Mpango amesema kuwa mchango wa hayati Benjamin Mkapa umeacha alama isiyofutika kwenye mageuzi ya kiuchumi, mapambano dhidi ya rushwa ambayo yalipelekea watanzania kumpa  jina la “Bwana Msafi”; mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi, kuhimiza uwazi na uwajibikaji katika utumishi wa Umma na usuluhishi wa migogoro ya kisiasa katika nchi za DRC, Burundi, Kenya.  

Amesema kuwa viongozi wanajifunza kutoka kwa Hayati Benjamin William Mkapa ujasiri na uthubutu wake katika kufanya maamuzi magumu kwa manufaa ya Taifa.

Aidha Makamu wa Rais Mpango, amesema hayati Mkapa ameacha alama ya   umuhimu wa kuwajibika na kusimamia misingi ya haki na usawa katika kuwahudumia wananchi wote. 

Hata hivyo Makamu wa Rais Mpango, amesema Hayati Benjamin William Mkapa alitambua kwamba Utegemezi una hatari nyingi na hivyo ni lazima kujizatiti kujitegemea kama nchi.

Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais amewataka wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Uviko 19 ambao umeingia katika wimbi la tatu lililo hatari Zaidi, pia amewasihi viongozi wa dini pamoja na waumini wa dini zote kumwomba Mungu msamaha ili afukuze ugonjwa huu duniani ili watu wake wamtukuze na kumwabudu kwa furaha na amani bila hofu ya Uviko 19.

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango  akiwasili kijijini Lupaso Wilaya ya Masasi kushiriki misa  ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha Hayati Benjamin William Mkapa, Julai 24, 2021.
Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango  pamoja na Mkewe mama Mbonimpawe Mpango wakiweka shada la maua katika kaburi la Hayati Benjamin William Mkapa, kijijini Lupaso wilayani Masasi, Julai 24,2021.
Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango  akipanda mti nyumbani kwa Hayati Benjamin William Mkapa mara baada ya kukamilika kwa misa ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha Hayati Benjamin William Mkapa, Julai 24,2021.

Coastal Union, Mtibwa Sugar zapeta Ligi Kuu 2021-22
Azam FC yatema maproo wanne