Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema ni muhimu nchi za Afrika zikashirikiana katika kuwezesha tafiti za ndani ya nchi ili kukabiliana na majanga mbalimbali yanapojitokeza pasipo utegemezi.

Dkt Mpango amesema hayo katika majadiliano maalum ya viongozi wakuu wa nchi za Afrika katika ajenda iliohusu namna Bara la Afrika linavyoweza kubadili utaratibu wa kimataifa katika kukabiliana na masuala mbalimbali.

Aidha, ameitaja taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) iliopo nchini Tanzania pamoja na taasisi zingine za ndani ya nchi zilitoa msaada mkubwa wakati wa kukabiliana na Uviko 19.

Amesema ni muhimu kushirikiana na sekta binafsi zilizopo ndani ya nchi kwani zimekua zikitoa mchango mkubwa hasa wakati wa kukabiliana na majanga mbalimbali.

Makamu wa Rais amesema kwa kutumia rasilimali zilizopo, mataifa ya Afrika yanaweza kukabiliana na changamoto zinazojitokeza na kuongeza kwamba kwa sasa Tanzania inazalisha chanjo ya mifugo hivyo hakuna budi mataifa ya Afrika kuungana katika uzalishaji huo utakaosaidia mahitaji ya baadae.

Mkutano huo umeshirikisha viongozi wakuu wa Nchi na Serikali za Afrika pamoja na wawakilishi kutoka mataifa hayo.

 

Ghana: Rais Samia apewa tuzo ya heshima
Uchinjaji Punda wasitishwa