Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imewatoa hofu wananchi kuhusu uvumi wa kuongezeka kwa deni la Taifa kwasababu deni hilo ni himilivu na liko chini ya ukomo wa hatari.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam  na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philipo Mpango wakati akitoa mwenendo wa  hali ya uchumi na utekelezaji wa bajeti  ya Serikali kwa mwaka 2017/2018.

Amesema kuwa katika tathmini iliyofanyika mwezi Novemba mwaka huu inaonyesha kuwa uwiano wa deni hilo na pato la Taifa ni asilimia 32.5 likilinganishwa na ukomo wa asilimia 56.

“Katika kuangalia ukomo wa deni hili ambao uko chini, inaonyesha kuwa deni hili ni himilivu  katika kipindi cha muda wa kati na muda mrefu”, amesema Dkt. Mpango

Hata hivyo, Mpango ameongeza kuwa Serikali tangu ifanikiwe kuziba mianya ya rushwa na ufisadi imefanikiwa kukusanya trilioni 1.2 kila mwezi na amewapongeza walipakodi nchini na kuwataka Watanzania kujenga tabia ya kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi.

Video: Anachokifanya Askofu Kakobe ni umburura- Gambo
Majaliwa avuna wanachama 60 kutoka upinzani