Tabibu Maarufu kwa jina la ‘Dkt. Mwaka’, ameeleza safari yake ya maisha hadi kuupata umaarufu katika tiba ya uzazi, ambapo amesema kuwa alianza kwa kufanya sanaa za maigizo pamoja na mazingaombwe.

Tabibu Mwaka ameeleza kuwa kabla hajaanza kujikita katika fani ya udaktari na kwenda kuongeza maarifa chuoni, alikuwa kijana mwenye kipaji cha kufanya mambo kadhaa akijihusisha na michezo ya maigizo, karate, sarakasi na mazingaombwe.

“Kweli niliwahi kuwa msanii, niliwahi kuigiza, nilikuwa na kikundi Ilala [Dar es Salaam] kwa Teacher. Na wakati huo nilikuwa nacheza karate na mwalimu wangu alikuwa anaitwa Migomba. Pia, nikawa muigizaji na akina Chekibudi miaka hiyo ya 2000,” Dkt. Mwaka ameiambia SnS.

“Ni kweli kwamba mimi ninapenda sanaa, na back then (enzi hizo) niliwahi kuwa mcheza sarakasi, niliwahi kuwa nachezea moto na nimewahi kuwa nafanya mazingaombwe. Vitu vyote hivyo ni vitu ambavyo nimewahi kupitia huko,” ameongeza.

Katika hatua nyingine, Mwaka amesimulia jinsi alivyoingia kwenye fani ya matibabu ya uzazi, akieleza kuwa ametokea kwenye familia ambayo ilikuwa imebobea kwenye tiba za asili na kwamba alikuwa akitumwa kutafuta mitishamba, kusaidia kuchanganya dawa na hata kushuhudia namna tiba husika inavyofanyika.

Aliongeza kuwa kushughulika na afya ya uzazi ilikuwa sehemu ya mambo aliyokuwa anayapenda tangu akiwa shule ya sekondari ambapo alikuwa akimsaidia mama yake kuchora kalenda ya mzunguko wa siku za kupata mtoto.

Amesema baada ya kufanya kazi za sanaa na baadaye biashara kadhaa, alikutana na mtu mmoja raia wa kigeni aliyesaidia kumtibu ndugu yake ambaye alikuwa anasumbuliwa na afya ya uzazi.

Amesema Matokeo ya tiba hiyo yalimfanya kupata kazi nyingi zaidi ughaibuni, na mwisho aliiona fursa hapa nchini akaenda kujiongezea elimu ya utabibu wa afya ya uzazi na kasha kufungua kituo cha kusaidia wanawake katika.

Mose Fan Fan wa 'Papa lolo' afariki dunia
Canelo kuzichapa ulingoni na Jacobs leo, nusura wazichape kavukavu