Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka Maafisa Utamaduni Mkoa na Wilaya kuwahimiza wadau wa Sekta ya Utamaduni kuwasilisha maoni yao ndani ya miezi mitatu.

Ametoa kauli hiyo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Saba wa Umoja wa Machifu nchini wenye lengo la kujadili namna ya kuhakikisha umoja huo unasajiliwa kisheria.

“Serikali iko katika mchakato wa kufanya maboresho ya Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997 ambayo imeonekana kuwa na mapungufu kulingana na hali ilivyosasa, hivyo basi nitoe rai kwenu Machifu kama wadau wakuu wa Sekta ya Utamaduni kutoa maoni yenu kwa haraka kwani yatasaidia kwa asilimia kubwa kuongeza ubora katika sera hii tunayoboresha na hivyo basi hakikisheni mnawasilisha maoni yenu kwa Maafisa Utamaduni ndani ya miezi hiyo,”amesema Dkt.Mwakyembe.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania Chifu, Frank Marrialle amesema kuwa umoja huo ulianza tangu mwaka 2014 na mpaka sasa una jumla ya wanachama 105 na kupitia umoja huo umekuwa ukisisitiza wajumbe wake kusimamia utunzaji mazingira pamoja usimamazi wa maadili katika jamii kwani machifu ndiyo mhimili wa kulinda utamaduni wa taifa.

 

 

 

Vyama vya Upinzani vyasusia uchaguzi Tanga
Waziri Mkuu amjulia hali Waziri Kigwangalla