Aliyekuwa Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema kuwa ushindi ambao wamekuwa wakiupata Chama Cha Mapinduzi hautokani na kupendelewa na Wakurugenzi ambao ni wasimamizi wa uchaguzi.

Ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache baada ya Mahakama kuu ya Tanzania kubatilisha sheria inayowapa Mamlaka Wakurugenzi kusimamia Uchaguzi huku baaadhi yao wakiwa wafuasi wa vyama vya siasa, kesi ambayo ilifunguliwa na Mwanaharakati Bob Chacha Wangwe.

Akijibu tamko la ACT – Wazalendo ambao walihoji juu ya CCM kupata ushindi wa upendeleo, Mwigulu Nchemba amesema kuwa ushindi wa CCM hautokani na hisani ya Wakurugenzi bali ni kura za wananchi.

“Ushindi wa CCM hautokani na hisani ya Wakurugenzi bali ni kura za wananchi. CCM ina heshima ya urithi wa ukombozi wa nchi hii ambayo chama kingine chochote hakina, CCM ina mtandao wa wanachama na muundo wa kitaasisi kuliko chama chochote kile nchini, CCM mara zote imekuwa na ilani bora, sera bora, na wagombea bora kuliko wengine”amesema Mwigulu

Hata hivyo, amwataka Wanasheria wafanye ya kisheria, hivyo wanasiasa wasitafute huruma na visingizio, wakati wengine hawana hata wanachama wanaofikia idadi ya wanachama wa CCM wa kijiji kimoja, hata wakisimamia wenyewe uchaguzi CCM ina wapiga kura na itashinda.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Mei 16, 2019
TRA Njombe yakusanya kiasi cha shilingi Bilioni 14.9