Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar tayari imefungua milango ya Uwekezaji.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo hii leo Machi 23, 2023 wakati alipokutana na wawekezaji kutoka Uingereza, wakiongozwa na Agnes Gitau kutoka Taasisi ya Eastern Africa Association na Amanda Van Dyke wa Kampuni ya ARCH, Ikulu mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Kufuatia hatua hiyo, Rais Dkt. Mwinyi amewataka Wawekezaji hao kuwekeza katika fursa zitokanazo na Uchumi wa Buluu, na hasa kwenye suala la uvuvi na vifaa vya kuhifadhia samaki .

Robertinho anasajili kimya kimya Simba SC
Geita Gold kupitia njia za Simba SC, Young Africans