Dkt. Faustine Ndugulile ameongoza katika kura za maoni za kuomba nafasi ya kuwania ubunge wa jimbo la Kigamboni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), uliofanyika leo, Julai 20, 2020.

Kwa mujibu wa matokeo rasmi ya kura hizo, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameshika nafasi ya pili akipata kura 122. Jumla ya kura zilizopigwa ni 399 na hakuna hata kura moja iliyoharibika.

Mchakato wa kura za maoni unaendelea katika majimbo mbalimbali nchini kwa vyama vya siasa, ambapo leo CCM waliendelea na mchakato katika maeneo mbalimbali, jimbo la Kigamboni likiwa miongoni mwa majimbo yaliyovuta usikivu wa watu wengi zaidi.

Watu wengi wamejitokeza katika mchakato huo ukilinaganisha na wakati mwingine wowote katika historia ya vyama vingi nchini. Katika mkoa wa Dar es Salaam pekee, wanachama 1,426 walichukua fomu ya kuomba kugombea nafasi ya ubunge, na 2,801 walichukua fomu ya kuwania kugombea nafasi ya udiwani.

Tulia, Zungu, Hawa Ghasia, Mhagama wapeta kura za maoni

Jafo, Lukuvi, Bashe waibuka kidedea kura za maoni

Fahamu yaliyopewa nafasi kwenye magazeti leo, Julai 21, 2020
Tulia, Zungu, Hawa Ghasia, Mhagama wapeta kura za maoni