Sekta ya afya nchini imetakiwa kujikita zaidi kwenye kuokoa na kuboresha afya ya mama mjamzito na mtoto ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa mradi wa Ukunga salama (More and Better Midwives) uliofanyika Wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

“Sisi sote tunafahamu umuhimu wa wauguzi na wakunga katika kuimarisha afya ya mama na mtoto hivyo Serikali ya awamu ya tano tumejipanga kuhakikisha kuwa tunapunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya mama na mtoto” alisema Dkt. Ndugulile.

Amesema kuwa Serikali inafahamu kuna changamoto ya upungufu wa watumishi katika kada mbalimbali za afya pamoja na nyinginezo na wanaendelea kuzifanyia kazi ikiwa ni kutoa kipaumbele cha ajira za wauguzi na wakunga.

Aidha, Dkt. Ndugulile amewaonya wakunga na wauguzi wenye tabia ya kutumia lugha chafu kwa wagonjwa pamoja na kuacha vitendo vya kuwaomba rushwa kwani fani hiyo inaendeshwa kwa taaluma na maadili.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Misungwi, Juma Sweda amesema kuwa wananchi wa wilaya hiyo wanatakiwa wawe mstari wa mbele katika kukata bima za afya kwani husaidia kuokoa gharama nyingi pindi wanapopata maradhi na mpaka hivi sasa wananchi wenye bima ta afya inakadiriwa ni 9100.

Naye Mkurugenzi wa Mradi wa Ukunga Salama nchini, Dkt. Julius Masanika amesema kuwa mradi huo utafadhili wanafunzi wa kanda ya ziwa na kanda ya magharibi wanaojiunga na vyuo vya Uuguzi na Ukunga wasio na uwezo kwa kuwalipia ada pamoja na mahitaji mengine.

 

Antonio Conte na Jose Mourinho watupiana vijembe
Video: Mungu alisema sitakufa - Tundu Lissu, Serikali yalipa madeni bil. 190/-