Balozi wa Tanzania, Dkt. Abdallah Saleh Possi, amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Papa Francis, Vatican.

Balozi Possi ambaye kituo chake cha kazi ni nchini Ujerumani katika mji wa Berlin pia utahudumia maeneo mengine tisa ya uwakilishi, ikiwemo Vatican.

Aidha, kabla ya kuwasilisha hati za utambulisho, Balozi Dkt. Possi alipata fursa ya kukutana na viongozi muhimu wa Vatican, wakiwemo Askofu mkuu, Paul Richard Gallagher, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje na ushirikiano wa kimataifa, Askofu Mkuu Angelo Becciu na Katibu Mkuu Msaidizi wa Vatican.

Hata hivyo, baada ya uwasilishaji hati, Balozi Dkt. Possi alipata fursa ya kukutana na jumuiya ya Watanzania waishio Vatican. na kuwaeleza kuwa wana jukumu kubwa la kutumia, nafasi zao kuhakikisha nchi ya Tanzania inadumu katika misingi ya uadilifu, umoja na amani ambavyo ni misingi muhimu ya maendeleo.
​

​

Gigy Money atoboa siri nzito kuachana na baba mtoto wake
Mstaafu 1, ajira 1, wahitimu 100,000 Nini kifanyike?