Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango amepokea tuzo ya shukrani kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi Angelina Ngalula.

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango (kushoto), akipokea tuzo ya shukurani kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi. Angelina Ngalula. (kulia).

Tuzo hiyo, imetolewa maalum kwa kutambua mchango wa Rais katika mafanikio ya sekta binafsi nchini katika hafla iliyofanyika wakati wa maadhimisho ya siku ya Sekta Binafsi jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais akitoa tuzo kwa washiriki mbalimbali wa hafla hiyo.

Miongoni mwa Viongozi wengine waliohudhuria utoaji wa tuzo hiyo ni pamoja na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki.

Baadhi ya washiriki katika maadhimisho hayo.
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Decemba 4, 2022
Huduma bora kwa walemavu ni lazima: Serikali