Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza jinsi alivyopokea kwa furaha taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya kuendelea kukua kwa uchumi wa Zanzibar.

Dk. Shein ameyasema hayo Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga ambapo katika mazungumzo hayo gavana amemueleza Dk. Shein jinsi uchumi wa Zanzibar unavyoendelea kuimarika.

Dk. Shein alimueleza kiongozi huyo kuwa hiyo ni habari njema ambayo inatoa mwanga wa maendeleo ya uchumi  Zanzibar kwani juhudi za makusudi bado zinaendelea kuchukuliwa katika kuhakikisha uchumi unaimarika.

Rais Dk. Shein ameongeza kuwa hatua hiyo imefikiwa kutokana na uwepo wa uongozi bora sambamba na mashirikiano mazuri yaliopo kati ya Serikali, wananchi pamoja na na Benki kuu ya Tanzania (BoT).

Mataifa ya G7 yajipanga na athari za Corona
Njia mbadala yabainishwa wakati wa matengenezo ya daraja Morogoro