Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba na Sheria, Deus Kibamba amemshauri Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein kutohudhuria Bungeni leo wakati rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt John Magufuli atakapolihutubia Bunge ili kuepusha kutokea tafrani.

Kibamba ametoa ushauri huo jana na kueleza kuwa kuna uwezekano mkubwa wabunge wa Ukawa wakaanzisha tafrani na kuharibu hali hali ya utulivu katika tukio hilo la kihistoria.

“Katiba yetu haisemi kwamba ni lazima Rais wa Zanzibar aweze kuwepo Bungeni, kwanza Rais wa Zanzibar sio sehemu ya Bunge la Muungano. Siku za nyuma wakati wa shamrashamra alikuwa anaalikwa kama mgeni mualikwa, mgeni muhimu aweze kushiriki katika sherehe hizo za kuzindua Bunge,” alisema Kibamba.

“Lakini kwa sasa hivi ningependa kama mchambuzi, ili kuepusha tafrani, ili kuepusha kuharibu sherehe, ningependekeza kwamba mheshimiwa Rais Ali Shein apumzike, abaki Zanzibar. Asiingi Bungeni kwa sababu hiyo itachafua hali ya hewa ambayo hatujui Ukawa watafanya nini, lakini nachojua wakatachofanya lazima kitaleta tafrani.”

CUF waandamana jijini London, Zanzibar washangaa uteuzi wa Waziri Mkuu
Ukawa Watahadharishwa Kuheshimu Hotuba Ya Rais Leo