Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, ameweka udongo katika jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za Ikulu akishuhudiwa na makamo mwenyekiti wa CCM Tanzania bara, Philp Mangula na Dkt. Bashiru Ally Kakurwa katibu mkuu wa CCM leo tarehe Juni 3, 2020 Ikulu ya chamwino Dodoma.

Dkt Shein, amempongeza Rais Magufuli kwa hatua aliyofikia ya ujenzi wa Ikulu ya Dodoma na kumtakia kila la heri katika safari yake hiyo na kuongeza kuwa hiyo ndiyo raha ya kujitawala kwakuwa inakupa nafasi ya kufanya vitu kwa uhuru.

Ameyafanya hayo mara baada ya kumaliza kikao cha ndani na mwenyeji wake Rais Magufuli kilichofanyika Chamwino na kusisitiza kuwa ofisi hiyo ni kwaajili ya wananchi wa Tanzania.

“Huko ndiyo kujitawala, kutawaliwa sio kuzuri na anayekutawala anafanya anavyotaka yeye kwa utashi wake pale anapotaka kufanya, tunapochukua hatua ya kujitawala wenyewe tunafanya mambo kama haya makubwa kwa ajili ya wananchi, hii ni ofisi kwa ajili ya wananchi wa Tanzania”¬†amesema Dkt Shein.

Simba SC yamkana Shonga
Wadau watoa maoni kuelekea kwenye mabadiliko Young Africans