Katibu Mkuu wa zamani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt. Wilbrod Slaa amewataka wananchi wa Tanzania kuacha kuijadili taarifa ya CAG kwa kuwa bado inaitwa ni taarifa ya awali na kuendelea kuijadili ni kuleta upotoshaji.

Akizungumza hivi karibuni kwenye mahojiano maalum na Dar24 Media nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, Dkt. Slaa amesema ni muhimu kuachia Kamati ya Bunge iwaite na kuwahoji maafisa waliotajwa ili kujua kama ni wizi au uwajibikaji.

“CAG akishawakabidhi taarifa yake, ikakabidhiwa kwa Rais na ikawasilishwa Bungeni kwa ule utaratibu uliowekwa baada ya siku 7 za Rais kupokea, ile Taarifa haiko for public discussion haipaswi kujadiliwa kwa sababu zile ni taarifa za awali. Saa hizi watu wanazungumza kwamba kuna upotevu wa trilioni 5.8, ‘Huu ni upuuzi mtupu‘ kwa sababu sasahivi ni ile kamati ya Bunge ndio inatakiwa kuwaita wale maafisa wa hesabu waliotajwa ndio waulizwe eleza hii, eleza hapa na hapa ili wajulikane kama ilikua ni wizi au uwajibikaji, kwa sabatu kuna mahali pengine ilikua ni risiti tu haionekani, kuna sehemu nyingine ni taarifa tu fulani haipo ila ikipatikana, ile taarifa inafutwa kwenye ripoti” amesema.

“Nadhani Zitto angesaidia sana hili taifa kwa kuwa muwazi na mkweli, Mimi na Zitto tulishiriki katika kutengeneza sheria ambayo inasimamia ukaguzi wa fedha katika nchi hii inaitwa Sheria ya ‘Audit ya 2009’ na niseme kwamba tulichangia kwa sehemu kubwa sana hata maneno ambayo yamewekwa mule ndani yametoka kwangu na Zitto,” ameongeza Dkt. Slaa.

Dkt. Slaa amempa lawama pia CAG kwa kutoa taarifa kwa kuingia kwa undani zaidi na kutaja namba halisi bali alitakiwa kusoma kwa ufupi ili majadiliano yakishamalizika ya kamati ya Bunge na marekebisho kufanyika ndio atoe taarifa kamili.

“CAG mwenyewe alihusika kuongeza hii taharuki, kwa kawaida inapotolewa hii taarifa yake haingii ‘into details’ kabla hii tariff haijafika kwa kamati ya Bunge na kujadiliwa. kwa sababu inapotoka huko unaweza kukuta robo tatu ya ile taarifa imefutwa. Ni wakati mzuri wa taifa kujua ile taarifa lakini ili ijadiliwe ni lazima maafisa hawa wa hesabu waitwe na Zitto anajua haya yote ndio maana nasema hata Yeye anatoa ‘analysis’ ambayo ni ‘premature’,” aliongeza Dkt. Slaa.

Amesema kwa kuijadili taarifa hiyo ya awali na kiasi ambacho kimetajwa cha Sh Trilioni 5.8 ni kumaanisha Kuwa Nchi yote imeharibika kwa rushwa na wizi.

Tazama mahojiano hayo maalumu kwa undani wa tarifa zaidi

Ahmed Ally: Mashabiki Simba SC watafutwa machozi Jumamosi
Mbunge atoa Swadaka ya FUTARI kwa wananchi