Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa bunge halikukataa  hoja binafsi ya Elimu bure, pedi bure ya Mbunge wa Viti Maalum wa Chadema Mkoa wa Geita, Upendo Peneza bali mchakato wa hoja hiyo ndiyo haukufikishwa ili ujadiliwe.

Amesema kuwa pamoja na kwamba hoja ya Mh. Peneza ilikuwa nzuri lakini mchakato wa kuwasilisha ndio haukukamilika.

“Sisi bungeni hoja binafsi lazima uzungumze na wabunge wengi ili wakuunge mkono. Hoja ya Peneza ni nzuri lakini haikupitia bungeni kujadiliwa, mchakato wa hoja hii haukuletwa bungeni halafu ukakataliwa,”amesema Dkt. Tulia

Hata hivyo, wiki iliyopita Mbunge, Peneza alijaribu kupeleka hoja binafsi kuhusu wanafunzi wa kike kupatiwa pedi lakini hoja hiyo haikufanikiwa kwani hoja hiyo ilikataliwa kwa sababu ilikuwa inavunja ibara ya 99 (2) ya Katiba.

Video: Hali ya kisiasa nchini ni tete- Sakaya
Serikali yabaini njia zinazotumiwa kupitisha dawa za kulevya

Comments

comments